Kutatua kwa Ripoti ya Muunganisho wa Mtandao
Muunganisho wa Wi-Fi
Jinsi ya kutatua hali yako ya mtandao au matatizo ya muunganisho
- Angalia Ripoti ya Muunganisho wa Mtandao ambayo ulichapisha. Kagua vipengee kwenye A (Check Network Connection (Kagua Muunganisho wa Mtandao)) ambao hali inaonyesha FAIL (IMESHINDWA).
- Katika orodha ya Vipengele vya Kukagua, bofya vipengele ambavyo vinaonyesha hali ya FAIL (IMESHINDWA) ili uonyeshe suluhisho.
- Kagua ujumbe ulioonyeshwa katika B na utafute ujumbe mmoja uliorodheshwa chini ya kila Kipengele cha Kukagua. Kisha fuata suluhisho.
Kwa ujumbe wenye * katika B, angalia "Kuhusu mazingira ya mtandao wako" kwa maelezo zaidi.
Vipengele vya Kukagua
Bofya vipengele hapa chini ili uende kwenye ujumbe na suluhisho.
- Wireless Network Name (SSID) Check (Ukaguzi wa Jina la mtandao Pasi waya (SSID))
- Communication Mode Check (Ukaguzi wa Modi ya Mawasiliano)
- Security Mode Check (Ukaguzi wa Modi ya Usalama)
- MAC Address Filtering Check (Ukaguzi wa Kuchuja Anwani ya MAC)
- Security Key/Password Check (Ukaguzi wa Ufunguo/Nenosiri la Usalama)
- IP Address Check (Ukaguzi wa Anwani ya IP)
- Detailed IP Setup Check (Ukaguzi wa Kindani wa Usanidi wa IP)
Ujumbe na suluhisho za vipengele vya kukagua
1. Wireless Network Name (SSID) Check (Ukaguzi wa Jina la mtandao Pasi waya (SSID))
| Nambari. |
Ujumbe |
Suluhisho |
| 1 |
No wireless network names (SSID) found (Hakuna majina ya mtandao pasi waya (SSID) yaliyopatikana). Confirm that the router/access point is turned on and the wireless network (SSID) is set up correctly (Thibitisha kwamba kipangishi njia/eneo la ufikiaji limewashwa na mtandao pasi waya (SSID) umewekwa vizuri). Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi). |
- Kagua kwamba eneo la ufikiaji limewashwa. Ikiwa kimezimwa, kiwashe na kisha utekeleze tena usanidi wa mtandao.
- Weka printa yako karibu na eneo la ufikiaji.
- Ikiwa umeingiza kwa mkono jina la mtandao pasi waya (SSID), thibitisha kwamba jina la mtandao wako pasi waya (SSID) liko sahihi. Ikiwa sio sahihi, liweke tena. Jina la mtandao wako pasi waya C (Hali ya Mtandao) chini ya Jina la Mtandao (SSID).
- Ikiwa umesanidi mtandao kwa kutumia WPS, kagua kama eneo lako la ufikiaji linakubali WPS.
- Ikiwa unataka kusanidi muunganisho wa Dharura, unahitaji kusanidi kwanza Dharura kwa Kompyuta yako. Tekeleza usanidi Dharura wa kompyuta yako na kisha utekeleze usanidi wa mtandao wa printa yako tena.
|
| 2 |
No wireless network names (SSID) found (Hakuna majina ya mtandao pasi waya (SSID) yaliyopatikana). Confirm that the wireless network name (SSID) of the PC you wish to connect is set up correctly (Thibitisha kwamba jina la mtandao pasi waya (SSID) la kompyuta unayotaka kuunganisha imewekwa vizuri). Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi). |
- Kagua kwamba kompyuta unayotaka kuunganisha imewashwa. Ikiwa imezimwa, iwashe na kisha utekeleze tena usanidi wa printa yako.
- Weka printa yako karibu na kompyuta unayotaka kuunganisha.
|
Ujumbe hapa juu huonyeshwa wakati jina la mtandao pasi waya (SSID) au uliowekwa haujapatikana wakati wa usanidi wa mtandao.
SSID ni jina la mtandao wako wa Wi-Fi. Ikiwa unatumia eneo la ufikiaji, basi mtandao wako tayari una jina wakati eneo la ufikiaji lilisanidiwa.
Ikiwa unataka kuunganisha printa yako na kompyuta moja kwa moja bila eneo la ufikiaji (muunganisho wa Dharura), unahitaji kusanidi mtandao wa Dharura wa kompyuta yako. Katika hali hii, unahitaji kuunda SSID kwenye kompyuta yako.
Ikiwa hujui SSID yako, tunapendekeza kwamba uwasiliane na mtu au kampuni ambayo ilisanidi mtandao wako.
Pia, unahitaji kuweka printa yako karibu na eneo la ufikiaji (au kompyuta) wakati wa usanidi ili printa yako ipokee ishara wazi kutoka kwa eneo la ufikiaji au kompyuta.
2. Communication Mode Check (Ukaguzi wa Modi ya Mawasiliano)
| Nambari. |
Ujumbe |
Suluhisho |
| 3 |
Wi-Fi communication mode (IEEE802.11*) does not match the current setting of the printer (Modi ya mawasiliano ya Wi-Fi (IEEE802.11*) hailingani na mpangilio wa sasa wa printa). Set the same communication mode to the printer, router/access point, and PC (Weka modi sawa ya mawasiliano kwenye printa, kipangishi njia/eneo la ufikiaji, na kompyuta). Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi).
*Uonekanaji wake hutofautiana kulingana na eneo lako. |
- Kagua kwamba modi ya mawasiliano ya Wi-Fi iliyowekwa kwa eneo la ufikiaji inalingana na inayokubaliwa na printa yako.
|
Ujumbe huu huonyeshwa wakati modi ya muunganisho wa Wi-Fi imewekwa kwa eneo la ufikiaji na kompyuta haikubaliwi na printa.
3. Security Mode Check (Ukaguzi wa Modi ya Usalama)
| Nambari. |
Ujumbe |
Suluhisho |
| 4 |
Security mode (e.g. WEP, WPA) does not match the current setting of the printer (Modi ya usalama (k.m. WEP, WPA) hailingani na mpangilio wa sasa wa printa). Confirm security mode (Thibitisha modi ya usalama). Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi). |
Thibitisha kwamba eneo la ufikiaji linatumia moja ya misimbo ifuatayo ya usalama. Ikiwa haitumii, tekeleza tena usanidi wa mtandao na uubadilishe kuwa msimbo unaokubaliwa wa usalama.
- WEP-biti 64 (biti 40)
- WEP-biti 128 (biti 104)
- WPA PSK (TKIP)
- WPA2 PSK (TKIP)
- WPA PSK (AES)
- WPA2 PSK (AES)
- WPA (TKIP/AES)
- WPA2 (TKIP/AES)
|
Ujumbe huu huonyeshwa wakati misimbo ya usalama imewekwa kwa vifaa vya mtandao na havikubaliwi na printa au havilingani na modi ya usalama ya printa.
Kuna aina tofauti za seti ya usalama kwa vifaa vya mtandao kulingana na mbinu yao ya nguvu au usimbaji fiche.
Modi za usalama zinazokubaliwa zinaweza kutofautiana kulingana na kifaa cha mtandao. Ili kuruhusu mawasiliano, msimbo huo wa usalama umewekwa kati ya kifaa cha mtandao na printa.
4. MAC Address Filtering Check (Ukaguzi wa Kuchuja Anwani ya MAC)
| Nambari. |
Ujumbe |
Suluhisho |
| 5 |
MAC address of your printer may be filtered (Anwani ya MAC ya printa yako inaweza kuchujwa). Check whether your router/access point has restrictions such as MAC address filtering (Kagua kama kipangishi njia/eneo lako la ufikiaji lina vizuizi kama vile uchujaji anwani ya MAC).
See the documentation of the router/access point or contact your network administrator for assistance (Angali nyaraka za kipangishi njia/eneo la ufikiaji au wasiliana na msimamizi wa mtandao wako kwa usaidizi). |
- Angalia mwongozo wa maagizo ambao ulikuja na eneo lako la ufikiaji kwa maelezo zaidi kuhusu kitendaji cha uchujaji anwani ya MAC. Ikiwa kitendaji cha kuchuja kimewashwa, sajili anwani yako ya MAC ya printa ili kuzuia printa yako dhidi ya kuchujwa.
- Ikiwa umetumia msimbo wa usalama wa WEP wa eneo lako la ufikiaji ili kuwasha uhalalishaji Ulioshirikiwa, thibitisha kwamba ufunguo wa uhalalishaji na kiolezo kiko sahihi.
|
Ujumbe huu huonyeshwa wakati uchujaji wa anwani ya MAC umewashwa na anwani ya MAC ya printa imesajiliwa kwenye eneo la ufikiaji.
Anwani ya MAC ni nambari ya utambulisho inayotumiwa kutambua kila kifaa cha mtandao.
Eneo la ufikiaji lina kitendaji ambacho hukuwezesha kuruhusu au kukataa ufikiaji wa kifaa kwenye mtandao kulingana na anwani yake ya MAC.
Ikiwa kitendaji hiki kimewashwa, vifaa vya mtandao tu vyenye anwani zilizosajiliwa za MAC ndizo zinazoweza kuunganishwa kwenye mtandao.
5. Security Key/Password Check (Ukaguzi wa Ufunguo/Nenosiri la Usalama)
| Nambari. |
Ujumbe |
Suluhisho |
| 6 |
Entered security key/password does not match the one set for your router/access point (Ufunguo/nenosiri lililowekwa la usalama halilingani na lile lililowekwa kwa kipangishi njia /eneo lako la ufikiaji). Confirm security key/password (Thibitisha ufunguo/nenosiri la usalama). Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi). |
Seti ya funguo za usalama za eneo la ufikiaji na ufunguo ulioingizwa wa usalama haulingani. Sanidi tena mtandao wako kwa kutumia ufunguo sahihi wa usalama. Ufunguo wa usalama unaathiriwa na ukubwa au udogo wa herufi. |
Ujumbe huu huonyeshwa wakati ufunguo wa usalama na seti ya ufunguo wa eneo lako la ufikiaji uliowekwa haulingani.
Ufunguo wa usalama (nenosiri) unafaa ili kuunganisha kwenye mtandao.
Ufunguo wa usalama unaathiriwa na ukubwa au udogo wa herufi. Ikiwa ufunguo ulioingizwa haulingani kabisa na ufunguo uliosajiliwa, muunganisho hushindwa.
6. IP Address Check (Ukaguzi wa Anwani ya IP)
| Nambari. |
Ujumbe |
Suluhisho |
| 7 |
Incorrect IP address is assigned to the printer (Anwani isio sahihi ya IP imewekwa kwenye printa). Confirm IP address setup of the network device (hub, router, or access point) (Thibitisha usanidi wa anwani ya IP ya kifaa cha mtandao (kitovu, kipangishi njia, au eneo la ufikiaji)). Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi).
|
- Kagua kama kitendaji cha DHCP cha eneo la ufikiaji kimewashwa. Ikiwa kimezishwa, kibadilishe hadi kimewashwa.
- Ikiwa umeweka anwani ya IP kwa mikono, anwani ya IP iko nje ya masafa yanayokubaliwa (batili). Ingiza anwani sahihi ya IP.
|
7. Detailed IP Setup Check (Ukaguzi wa Kindani wa Usanidi wa IP)
| Nambari. |
Ujumbe |
Suluhisho |
| 8 |
Confirm the connection and network setup of the PC or other device (Thibitisha usanidi wa muunganisho na mtandao wa kompyuta au kifaa kingine).
Connection using the EpsonNet Setup is available (Muunganisho kwa kutumia EpsonNet Setup unapatikana).
Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi).
| - Kagua zifuatazo:
- Kagua kwamba nishati ya vifaa imewashwa, kama vile kompyuta ambayo inataka kutumia printa.
- Kagua kwamba vifaa ambavyo vinataka kutumia printa, kama vile kompyuta, viko kwenye mtandao sawa.
- Ikiwa umekagua vipengele hapa juu, tekeleza usanidi wa mtandao kwa kutumia EpsonNet Setup.
|
| 9 |
Confirm IP address, subnet mask, and default gateway setup (Thibitisha anwani ya IP, anwani fiche, na usanidi wa njia msingi).
Connection using the EpsonNet Setup is available (Muunganisho kwa kutumia EpsonNet Setup unapatikana).
Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi).
| - Kagua zifuatazo:
- Vifaa vingine kwenye mtandao vimewashwa
- Anwani ya mtandao ya printa iliyowekwa kwa mikono ni sahihi
- Anwani ya mtandao ya printa ni sawa na ile nyingine ya vifaa vingine
- Ikiwa anwani ya mtandao sio sahihi, weka anwani sahihi kwa kutumia paneli ya LCD ya printa.
Ikiwa huwezi kubadilisha mipangilio kwa kutumia printa chako, wezesha mipangilio kwa kutumia EpsonNet Setup.
Anwani yako ya sasa ya IP, anwani fiche, na njia msingi huonyeshwa katika C (Hali ya Mtandao).
|
| 10 |
Setup is incomplete (Usanidi haujakamilika). Confirm default gateway setup (Thibitisha usanidi wa njia msingi).
Connection using the EpsonNet Setup is available (Muunganisho kwa kutumia EpsonNet Setup unapatikana).
Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wako wa mtandao kwa usaidizi).
| - Kagua zifuatazo:
- Anwani msingi ya njia imewekwa kwa mikono ni sahihi
- Kifaa kilichobainishwa kama njia msingi kimewashwa
- Ikiwa anwani msingi ya njia sio sahihi, weka anwani sahihi kwa kutumia paneli ya LCD ya printa.
Ikiwa huwezi kubadilisha mipangilio kwa kutumia printa chako, wezesha mipangilio kwa kutumia EpsonNet Setup.
Anwani yako ya sasa ya njia msingi imeonyeshwa katika C (Hali ya Mtandao) chini ya Njia Msingi.
|
| 11 |
Confirm the following (Thibitisha zifuatazo):
-Entered security key/password is correct (Ufunguo/nenosiri lililoingizwa la usalama ni sahihi)
-Index of the security key/password is set to the first number (Kiolezo cha ufunguo/nenosiri la usalama kimewekwa kwa nambari ya kwanza)
-IP address, subnet mask, or default gateway setup is correct (Anwani ya IP, barakoa ya mtandao mdogo, au usanidi wa njia msingi)
Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wa mtandao wako kwa usaidizi).
| - Kagua zifuatazo:
- Vifaa vingine kwenye mtandao vimewashwa
- Anwani ya mtandao ya printa iliyowekwa kwa mikono ni sahihi
- Anwani ya mtandao ya printa ni sawa na ile nyingine ya vifaa vingine
- Ikiwa umekagua vipengele vyote hapa juu, jaribu zifuatazo:
- Anzisha EpsonNet Setup kwenye kompyuta ambayo inatumia mtandao sawa kama printa.
Ikiwa printa yako imeorodheshwa katika orodha ya printa, weka anwani ya IP ya printa kwenye skrini ya usanidi wa anwani ya IP. Ikiwa printa yako imeorodheshwa, huenda ufunguo wa usalama sio sahihi. Tekeleza usanidi wa mtandao kwa kutumia paneli ya LCD ya printa na uingize ufunguo sahihi wa usalama.
- Unaweza kusajili funguo kadhaa za usalama kwa eneo la ufikiaji katika modi ya usalama ya WEP. Ikiwa funguo kadhaa zimesajiliwa, kagua kama umeingiza ufunguo wa kwanza uliosajiliwa.
|
| 12 |
Confirm the following (Thibitisha zifuatazo):
-Entered security key/password is correct (Ufunguo/nenosiri lililoingizwa la usalama ni sahihi)
-Index of the security key/password is set to the first number (Kiolezo cha ufunguo/nenosiri la usalama kimewekwa kwa nambari ya kwanza)
-Connection and network setup of the PC or other device is correct (Usanidi wa muunganisho na mtandao wa kompyuta au kifaa kingine ni sahihi)
Contact your network administrator for assistance (Wasiliana na msimamizi wa mtandao wako kwa usaidizi).
| - Kagua zifuatazo:
- Vifaa vya mtandao, kama vile modemu, kitovu, na kipangishi njia vimewashwa
- Anwani ya IP ya vifaa vya mtandao kando na printa imewekwa kwa mikono (Ikiwa anwani ya IP ya printa imepangiwa otomatiki lakini vifaa vingine vya mtandao vimewekwa kwa mikono, huenda mtandao wa printa ukatofautiana na vifaa vingine vya mtandao)
- Ikiwa umekagua vipengele vyote hapa juu, jaribu zifuatazo:
- Anzisha EpsonNet Setup kwenye kompyuta ambayo inatumia mtandao sawa kama printa.
Ikiwa printa yako imeorodheshwa katika orodha ya printa, weka anwani ya IP ya printa kwenye skrini ya usanidi wa anwani ya IP. Ikiwa printa yako imeorodheshwa, huenda ufunguo wa usalama sio sahihi. Tekeleza usanidi wa mtandao kwa kutumia paneli ya LCD ya printa na uingize ufunguo sahihi wa usalama.
- Unaweza kusajili funguo kadhaa za usalama kwa eneo la ufikiaji katika modi ya usalama ya WEP. Ikiwa funguo kadhaa zimesajiliwa, kagua kama umeingiza ufunguo wa kwanza uliosajiliwa.
|
Kagua anwani ya IP ya kichapjshi na ukague kama printa ya mtandao inaweza kufikia vifaa vingine kwenye mtandao. Katika hali nyingine, hitilafu haiwezi kubainishwa. Tunapendekeza kutekeleza usanidi wa mtandao kwa kutumia EpsonNet Setup.
Kuhusu anwani za mtandao:
Anwani ya IP haiashirii tu kwamba vifaa vimeunganishwa kwenye mtandao kama vile kompyuta, kitovu, na kipangishi njia lakini pia masafa yao ya mtandao. Vifaa kwenye mtandao sawa vinaweza kuwasiliana na vile vingine. Ikiwa unataka kuwasiliana na vifaa kwenye mtandao tofauti, kipangishi njia kinahitajika. Anwani ya IP ina sehemu mbili. Sehemu ya kwanza inaitwa "anwani ya mtandao" na huashiria masafa ya mtandao. Sehemu ya pili inaitwa "anwani ya upangishaji" na huashiria kifaa cha mtandao. Mstari kati ya anwani ya mtandao na anwani ya upangishaji hutofautiana kulingana na mizani (darasa) la mtandao. Hata hivyo unaweza kufasili mstari kati ya anwani ya mtandao na anwani ya upangishaji kwa kutumia anwani fiche.
Ikiwa unatumia printa yako kwenye mtandao wa nyumbani, weka mpangilio wa anwani ya IP ya kipangishi kwa "Otomatiki" wakati unatumia kitendaji cha ufikiaji eneo la ufikiaji la DHCP. Ikiwa unataka kutumia "Kwa mikono" ili kuweka anwani ya IP ya printa, angalia zifuatazo ili uweke anwani ya IP na anwani fiche.
- Kagua anwani ya IP ya kipangishi njia, (au eneo la ufikiaji) lililounganishwa kwenye kompyuta yako. Kwa maelezo, angalia mwongozo wa maagizo wa kipangishi njia (au eneo la ufikiaji).
- Anwani zote za IP zimeandikwa katika vipande vya thamani nne za nambari (kwa IPv4). Katika sehemu ya mwisho, weka thamani za kipekee za nambari katika masafa ya 1 hadi 254. (Wakati kipangishi njia ni seva ya DHCP au wakati kuna seva nyingine ya DHCP katika mtandao wa nyumbani, weka thamani ambayo haizozani na anwani ya IP iliyowekewa seva ya DHCP.)
Mfano wa mpangilio:
Anwani ya IP ya kipangishi njia (au eneo la ufikiaji): 192.168.1.
1
Mfano wa mpangilio kwenye printa: 192.168.1.
3
Ikiwa unatumia kipangishi chako katika mtandao mdogo,
255.255.255.0 huwekwa kwa vifaa vyote vya mtandao kwa barakoa ya mtandao mdogo. Pia, njia hutumia thamani sawa kama anwani ya IP ya eneo la ufikiaji.
Kuhusu mazingira ya mtandao
Na hata pia ripoti ya ukaguzi ya hali ya mtandao/muunganisho, ujumbe ufuatao huonyeshwa ili kukufahamisha mambo mengine katika mazingira ya mtandao wako ambayo yanahitaji kuboreshwa.
| Ujumbe |
Suluhisho |
| *Signal strength is low (Nguvu ya ishara iko chini). If you have problems printing or scanning, improve your wireless network environment (Ikiwa una matatizo ya kuchapisha au kuchanganua, boresha mazingira ya mtandao wako pasi waya). |
Kwa sababu ya nguvu kidogo ya ishara, huenda kasi ya uchapishaji ikawa polepole au uchapishaji huenda ukatatizwa.
Tekeleza yafuatayo ili uboreshe mazingira:
- Weka printa karibu na eneo la ufikiaji
- Ondoa vizuizi vyovyote kati ya eneo la ufikiaji na printa.
|
| *A router/access point channel conflict has been detected (Mzozo wa kituo cha kipangishi njia/eneo la ufikiaji umetambuliwa). If you have problems printing or scanning, improve your wireless network environment (Ikiwa una matatizo ya kuchapisha au kuchanganua, boresha mazingira ya mtandao wako pasi waya). |
Mwingiliano wa ishara unaweza kusababishwa na mitandao mingine isiyotumia waya inayotumiwa katika vyumba au majengo yaliyo karibu. Kuweka printa karibu na eneo la ufikiaji huenda ukaboresha mazingira. |
| *Signal strength is low (Nguvu ya ishara iko chini). A router/access point channel conflict has been detected (Mzozo wa kituo cha kipangishi njia/eneo la ufikiaji umetambuliwa). If you have problems printing or scanning, improve your wireless network environment (Ikiwa una matatizo ya kuchapisha au kuchanganua, boresha mazingira ya mtandao wako pasi waya). |
Kwa sababu ya nguvu kidogo ya ishara, huenda kasi ya uchapishaji ikawa polepole au uchapishaji huenda ukatatizwa. Mwingiliano wa ishara unaweza kusababishwa na mitandao mingine isiyotumia waya inayotumiwa katika vyumba au majengo yaliyo karibu.
Tekeleza yafuatayo ili uboreshe mazingira:
- Weka printa karibu na eneo la ufikiaji
- Ondoa vizuizi vyovyote kati ya eneo la ufikiaji na printa.
|
| *Multiple network names (SSID) that match your entered network name (SSID) have been detected (Majina kadhaa ya mtandao (SSID) ambayo yanalingana na jina lako la mtandao uliloingiza (SSID) yamegunduliwa). Confirm network name (SSID) (Thibitisha jina la mtandao (SSID)). |
Unaunganisha kwenye eneo tofauti la ufikiaji.
Jaribu yafuatayo:
Badilisha SSID ya eneo la ufikiaji ambalo unataka kuunganisha, na kisha utekeleze tena usanidi wa mtandao wa printa yako.
|
| *No more devices can be connected (Hakuna vifaa zaidi vinavyoweza kuunganishwa). Disconnect one of the connected devices if you want to add another one (Tenganisha moja ya vifaa vilivyounganishwa ikiwa unataka kuongeza kifaa kingine). |
Ikiwa unataka kuongeza kifaa kipya, tenganisha kifaa kimoja cha vifaa vya sasa kwa kutumia mipangilio ya Wi-Fi ya kifaa, au tenganisha vifaa vyote kwa kubadilisha nenosiri kutoka kwenye printa yako. |