Kwa kila mtu hadi umri wa miaka 16:
Tafadhali tazama ukurasa huu pamoja na mzazi au mlezi, kama vile baba au mama.
Ukurasa huu hutoa maelezo kuhusu tovuti ifuatayo (kuanzia sasa kuendelea inarejelewa kama "tovuti") inasimamiwa na kuendeshwa na Seiko Epson Corporation (kuanzia sasa kuendelea inarejelewa kama "kampuni").
- https://support.epson.net
Tafadhali kumbuka kwamba hatukusanyi maelezo yoyote ya kibinafsi (maelezo ambayo yanaweza kutumiwa kutambua watu) kutoka kwenye wageni kwenye tovuti hii.
1. Upana wa Taarifa hii ya Faragha
1-1. Upana
Taarifa hii ya Faragha (kuanzia sasa kuendelea inarejelewa kama "taarifa") hutumika kwenye historia yako ya kuvinjari kwenye tovuti (ikijumuisha tabia yako ya kuvinjari, maelezo kuhusu kifaa chako na mengine zaidi).
1-2. Kipaumbele cha vipengee vinavyodhaminiwa kuangaziwa kimadhubuti
Ikiwa sehemu kwenye tovuti hii inaelezea sera kwa udhahiri au mambo muhimu ambayo yanatofautiana na taarifa hii, hizo sheria na masharti zitapewa kipaumbele.
2. Upataji maelezo na madhumuni ya matumizi unapofikia tovuti hii
Tovuti hii hutumia Google Analytics zinazotolewa na Google LLC. Ili kupata maelezo yafuatayo.
Tafadhali rejelea URL iliyo kwenye upande wa kulia (https://policies.google.com/privacy) ili kupata maelezo ya jinsi data inatumiwa na Google LLC.
- Maelezo kuhusu matumizi hayatambui watu (mionekano ya ukurasa, mionekano ya video, viungo kutoka kwenye tovuti hii na mengine zaidi): kwa ajili ya uchambuzi wa kitakwimu na uboreshaji wa huduma.
- Maelezo kuhusu kifaa chako (OS, kivinjari, lugha, eneo na mengine zaidi): kwa ajili ya uchambuzi wa kitakwimu ya mazingira ya matumizi na uboreshaji wa huduma.
Google Analytics hutumia vidakuzi vya wahusika wa kwanza ili kurekodi maelezo kuhusu jinsi unatumia tovuti.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu kutoshiriki kwenye Google Analytics, tafadhali rejelea kwenye tovuti hii.
https://tools.google.com/dlpage/gaoptout/
Ikiwa unataka kuzuia vidakuzi visifuatilie matumizi yako na visipate maelezo yako, tazama Kifungu cha 3 “Kukataa vidakuzi”.
3. Kukataa vidakuzi
Vivinjari vingi sana hukubali vidakuzi kiotomatiki kwa chaguo msingi. Vidakuzi kwenye kifaa chako vitasalia kwenye kifaa chako hadi uvifute au hadi muda wavyo uishe, lakini unaweza kuvilemaza kwa kubadilisha mipangilio katika kivinjari chako. Hata hivyo, tafadhali kumbuka kwamba ikiwa utazima vidakuzi, unaweza kukumbana na matatizo kama vile kutoweza kutumia vipengele fulani vya tovuti hii au baadhi ya kurasa hazitaonyeshwa vizuri.
Ili kupata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya kidakuzi, tafadhali rejelea mwongozo wa kivinjari chako.
4. Kushughulikia viungo kutoka kwenye tovuti hii
Taarifa hii haitumiki kwenye tovuti zingine zilizounganishwa kutoka kwenye tovuti hii. Rejelea tovuti husika ili kupata maelezo kuhusu jinsi tovuti hizi zinashughulikia maelezo ya kibinafsi.
5. Maswali kuhusu taarifa hii
Ili kuuliza maswali na kuwasilisha malalamiko kuhusiana taarifa hii, unaweza kuwasiliana nasi kupitia anwani ifuatayo ya baruapepe.
- Sehemu ya Mwasiliani
- Msimamizi wa ulinzi wa maelezo ya kibinafsi wa Programu ya Simu ya Epson (kwa ajili ya kichapishi) na tovuti ya support.epson.net
- Baruapepe: privacy.epsonmobileprintapps@exc.epson.co.jp
* Kwa vile hatuwezi kujibu maswali kuhusu matumizi au matatizo kuhusiana na tovuti hii au bidhaa, tafadhali rejelea maelezo ya mwasiliani yaliyotolewa kwa kila bidhaa kwa kila swali.
Ikiwa maelezo ya kibinafsi yanajumuishwa katika swali lako, tutayatumia tu kujibu swali lako na sio kwa azma nyingine.
6. Kutii sheria na kanuni na kusahihisha Taarifa ya Faragha
Tunadhibiti na kutumia maelezo ya kibinafsi kwa mujibu wa Sheria ya Japani kuhusu Ulinzi wa Maelezo ya Kibinafsi. Tunaweza kusahihisha Taarifa ya Faragha kila baada ya muda ili kutii mabadiliko katika sheria na kanuni, ili kuhakikisha ulinzi wa maelezo ya kibinafsi, au kwa ajili ya sababu zingine; kwa hivyo tunakuhimiza uangalie Taarifa ya Faragha mara kwa mara. Masasisho yoyote yaliyofanywa yatachapishwa kwenye tovuti hii.
Taarifa hii inatumika kuanzia tarehe ya kuchapishwa kwenye tovuti hii.
7. Historia ya kusahihisha
Iliundwa: Machi 27, 2024