MAKUBALIANO YA LESENI YA PROGRAMU YA MTUMIAJI WA MWISHO YA EPSON

NOTISI KWA MTUMIAJI: TAFADHALI SOMA MAKUBALIANO HAYA KWA MAKINI KABLA YA KUSAKINISHA AU KUTUMIA BIDHAA HII.

IKIWA UKO MAREKANI, FUNGU 19-23 LA HATI HII LINATUMIKA KWAKO. FUNGU 22 LINA MASHARTI YANAYOBANA YA UPATANISHI YANAYOPUNGUZA UWEZO WAKO KUTAFUTA USULUHISHI KATIKA MAHAKAMA MBELE YA HAKIMU AU JOPO LA WAAMUZI, NA YANAONDOA HAKI YAKO YA KUSHIRIKI KATIKA MASHTAKA YA KIKUNDI AU UPATANISHI WA KIKUNDI KWA MIZOZO FULANI. “CHAGUO LA KUJIONDOA” LINAPATIKANA KATIKA FUNGU 22.7 KWA WANAOTAKA KUTOJUMUISHWA KATIKA UONDOAJI WA HAKI YA UPATANISHI NA MASHTAKA YA KIKUNDI.

UKINUNUA BIDHAA HII NCHINI AUSTRALIA, FUNGU 24-36 ZA HATI HII ZINAWEZA KUTUMIKA KWAKO. FUNGU 25 NA 28 ZINAELEZEA WAKATI AMBAPO FUNGU HIZI ZINAWEZA KUTUMIKA. FUNGU 24-36 ZIMEBAINISHA ULINZI WA LAZIMA WA KISHERIA AMBAO HAUWEZI KUTENGWA CHINI YA SHERIA. PALE IMEANDIKWA, MASHARTI MENGINE KATIKA MAKUBALIANO HAYA NI KWA MUJIBU WA FUNGU 24-36.

Haya ni makubaliano ya kisheria (“Makubaliano”) kati yako (mtu binafsi au shirika, ukijulikana hapa kama “wewe”) na Seiko Epson Corporation (ikijumuisha washiriki wake, “Epson”) ya programu zinazoambatanishwa, zikijumuisha hati zozote husika, ngome, au usasisho (kwa pamoja zinajulikana hapa kama “Programu”). Programu hii inatolewa na Epson na wagavi wake kwa kutumiwa na bidhaa ambatani kipembezo cha kompyuta ya Epson (“Maunzi ya Epson”). KABLA YA KUSAKINISHA, KUNAKILI, AU VINGINEVYO, KUTUMIA PROGRAMU HII, UNAHITAJI KUPITIA NA KUKUBALI SHERIA NA MASHARTI YA MAKUBALIANO HAYA, IKIWA NI PAMOJA NA SERA YA FARAGHA YA EPSON iliyotajwa katika Fungu 17. Ikiwa unakubali, bofya kwenye kitufe cha Ninakubali (“NINAKUBALI”, “SAWA” au uwakilishaji wowote sawia wa kukubali) kilicho hapa chini kama kipo. Ikiwa hukubali sheria na masharti ya Makubaliano haya, bofya kwenye kitufe cha Sikubali (“TOKA”, “Ghairi” au uwakilishaji wowote wa kukataa) kama kipo na urudishe Programu, pamoja na pakiti na nyenzo husika, kwenye Epson au mahali uliinunua kwa marejesho kamili ya fedha.

1.Utoaji wa Leseni.
Kwa mujibu wa fungu 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), Epson inakupatia leseni yenye kikomo, isiyo ya kipekee ya kupakua, kusakinisha na kutumia programu kwa matumizi yako ya kibinafsi na ya ndani ya biashara kwenye diski kuu au vifaa vingine vya hifadhi vya kompyuta au kwa programu-tumizi (ambayo pia inajulikana kama “Programu”), kwenye simumahiri, kijilaptopu, au kifaa kingine cha mkononi (kwa pamoja vikijulikana hapakama, “Kifaa”), bora Programu hiyo inatumiwa (i) katika eneo moja pekee (k.m. Nyumbani au ofisini au mahali pa biashara), au kwa vifaa vya mkononi, kwenye Kifaa kinachomilikiwa au kudhibitiwa na wewe, na (ii) katika Maunzi ya Epson unayoyamiliki wewe pekee. Unaweza kuwaruhusu watumiaji wengine wa Maunzi ya Epson waliounganishwa kwenye mtandao wako kutumia Programu, bora uhakikishe kwamba watumiaji hao wanatumia programu hii kulingana na Makubliano haya pekee. Unakubali kuwajibika kwa na kufikia Epson kwa dhima inayotikana na matumizi ya watumiaji hao. Unaweza kuunda nakala-rudufu za Programu kama akiba, inavyohitajika, bora nakala hizo za akiba zinatumiwa tu kusaidizi mautmizi yako ya Maunzi ya Epson.

2.Uboreshaji na Usasisho.
Kwa mujibu wa fungu 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), ukinunua uboreshaji, au toleo lililosasishwa, toleo lililorekebishwa, au vipengele nyongeza kwa au vya Programu kutoka Epson, uboreshaji, toleo lililosasihwa, toleo lililorekebishwa, au nyongeza hiyo, itajumuishwa katika neno Programu na kutawaliwa na Makubaliano haya. Unakiri kwamba Epson haina wajibu wa kukupatia Usasisho wowote (kama ilivyofafanuliwa hapa chini katika Fungu hili 2) wa Programu. Hata hivyo, mara kwa mara, Epson inaweza, kutoa matoleo yaliyosasishwa ya Programu na Programu inaweza kuunganishwa kwenye Epson au seva za wahusika wa tatu kiotomatiki kupitia Wavuti kutafuta usasisho uliopo wa Programu, kama vile, urekebishaji wa hitilafu, viraka, uboreshaji, vipengele vya ziada au vipengele bora, programu-jalizi, na matoleo mapya (kwa pamoja, “Usasisho”) na inaweza (a) kusasisha toleo la Programu unalotumia kwenye kifaa chako cha kibinafsi kiotomatikali kielektronikali au (b) kukupatia uchaguzi wa kupakua Usasisho unaohitajika mwenyewe. Iwapo ulisakinishaji EPSON Software Updater vitofauti lakini hutaki kuruhusu Epson kutafuta usasisho unaopatikana wa Programu, unaweza kulemaza kipengele hiki kwa kusakinusha EPSON Software Updater. Kwa kusakinisha Programu hii na kukosa kulemaza utafutaji wowote otomatiki wa Usasisho, ikiwa inatumika, basi unakubali kuagiza na kupokea Usasisho kiotomatiki kutoka kwa Epson au seva za wahusika wa tatu, na kwamba sheria na masharti za Makubaliano haya yatatumia kwa Usasisho huu wote.

3.Haki na Vikwazo Vingine.
Unakubali kwamba hutarekebisha, kulinganisha, au kutafsiri Programu hii na unakubali hutajaribu kuiga, kuchambua msimbo, kutenganisha au vinginevyo, kujaribu kugundua msimbo-chanzo wa Programu hii. Huwezi kukodisha, kupangisha, kusambaza, kuazima Programu hii kwa wahusika wa tatu au kujumuisha Programu hii katika bidhaa au huduma inayozalisha kipato. Hata hivyo, unaweza kuhamisha haki zako zote za kutumia Programu hii kwa mtu mwingine au shirika lingine la kisheria, bora mpokeaji pia akubali sheria za Makubaliano haya na uhamishe Programu, ikiwa ni pamoja na nakala zote, usasisho, na matoleo yote ya awali, na Maunzi ya Epson, kwa mtu au shirika hilo. Leseni ya Programu hii inatolewa kama kitengo kimoja na programu zake vijenzi haviwezi kutenganishwa matumizi mengine. Zaidi ya hayo, unakubali kutoweka Programu hii kwenye au katika mazingira ya pamoja yanayoweza kufikiwa kupitia mtandao wa umma kama vile WAvuti au vinginevyo yanayoweza kufikiwa na watu wengine walio nje ya eneo moja lililotajwa katika Fungu 1 hapa juu.

4.Umiliki.
Hati ya kumiliki, haki ya umiliki, na haki za uvumbuzi ziliazo katika na kwenye Programu zitasalia na Epson au watoa leseni na wagavi wake. Programu hii inalindwa na Sheria ya Hakimiliki ya Marekani, sheria za hakimiliki za Japani na maafikiano ya kimataifa ya hakimiliki, pamoja na sheria na maafikiano mengine ya hakimiliki. Hakuna uhamishaji wa hati yoyote ya kumiliki au umiliki wowote wa Programu hii kwako na Leseni hii haifai kuchukuliwa kama uuzaji wa haki zozote za Programu. Unkaubali kwamba hutaondoa au kubadilisha hakimiliki yoyote, nembo yoyote ya kibinaishara, au alama yoyote ilisajiliwa na notisi zingine za umiliki zilizo kwenye nakala zozote za Programu hii. Epson na/au watoa leseni na wagavi wake wanahifadhi haki zote ambazo hazijapeanwa. Programu hii pia inaweza kuwa na taswira, vielelezo, miundo na picha (“Nyenzo”), na hakimiliki ya nyenzo hizo inamilikiwa na Epson na/au watoa leseni na wagavi wake, na inalindwa na sheria, mikataba na maafikiano ya kitaifa na/au kimataifa yauvumbuzi. Kwa udhahiri, (1) Nyenzo hizi zitatumiwa kwa madhumuni yasiyo ya kibinashara pekee, (2) Nyenzo hizi zitahaririwa, kurekebishwa na kubalikiwa kulingana na namna iliyobainishwa na Programu pekee, na (3) unaweza kutumia Nyenzo hizi kwa matumizi ya kisheria ya kibinafsi, ya nyumbani, au vinginevyo, yanayoruhusiwa kisheria.

5.Chanzo Huria na Vijenzi Vingine vya Wahusika wa Tatu.
Walakini toleo la leseni lililotajwa hapo awali, unakiri kwamba vijenzi fulani vya Programu vinaweza kusimamiwa leseni za wahusika wa tatu, ikiwa ni pamoja na leseni za programu za “chanzo huria”, ikimaanisha kwamba leseni zozote za programu zilizoidhinishwa kama leseni za chanzo huria na Open Source Initiative au leseni zozote sawia, ikijumuisha bila kikomo, leseni yoyote ambayo, kama masharti ya usambazaji wa programu iliyotolewa chini ya leseni kama hiyo, inahitaji msambazaji atoe programu hiyo katika umbizo la msimbo huria (kama vijenzi vya wahusika wa tatu, “Vijenzi vya Wahusika wa Tatu”). Orodha ya Vijenzi vya Wahusika wa Tatu, na maneno husika ya leseni (inavyohitajika), kwa matokeo fulani ya Leseni yameandikwa kwa https://support.epson.net/terms/, mwishoni mwa Makubaliano haya, mwongozo/CD muhimu ya mtumiaji, au taarifa ya leseni inayoonyeshwa kwenye Kifaa chako/katika Programu. Kwa kiwango kinachohitajika na leseni inayosimamia Vijenzi vya Wahusika wa Tatu, masharti ya leseni hizo yatatumika badala ya maneno ya Makubaliano haya. Kwa kiwango masharti ya leseni zinazotumika kwa Vijenzi vya Wahusika wa Tatu yanazuia vizuizi vyovyote vya Makubalianokuhusu Vijenzi hivyo vya Wahusika wa Tatu, vizuizi hivyo havitatumia kwa Kijenzi kama hivyo cha Wahusika wa Tatu.

6.Matokeo Mengi ya Programu.
Unaweza kupokea au kupata Programu hii katika matoleo zaidi ya moja (k.m. Kwa mazingira tofauti ya matumizi; matoleo ya lugha mbili au zaidi; yaliyopakuliwa kutoka kwenye seva ya Epson au kwenye CD-ROM), hata hivyo, bila kujali aina au idadi ya nakala unazopokea, bado unaweza kutumia media au toleo linalofaa la leseni iliyotolewa katika Fungu 1 hapa juu pekee.

7.Kikanusho cha Dhamana na Suluhisho.
Kwa mujibu wa fungu 25 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), ikiwa utanunua Programu hii kupitia media kutoka kwa Epson au mchuuzi, Epson inakuhakikishia kwamba media ambayo Programu imerekodiwa haina kasoro za ustadi na nyenzo katika matumizi ya kawaida kwa kipindi cha siku 90 kutoka tarehe ya kuwasilishwa kwako. Ikiwa media itarudishwa kwa Epson au mchuuzi aliyeiuza ndani ya siku 90 za tarehe ya kuwasilishwa kwako, na ikiwa Epson itaamua kwamba media hiyo ina kasoro na bora media iwe haikutumiwa vibaya, kutumiwa kwa njia isiyofaa au kutumwa katika kifaa kibovu, basi Epson itabadilisha media hiyo, baada ya wewe kurejesha Programu hiyo kwa Epson ikiwa na nakala zote za sehemu zozote. Unakiri na kukubali kwamba matumizi ya Programu hii ni kwa hatari yako peke yako. PROGRAMU HII INATOLWA “KAMA ILIVYO” NA BILA DHAMANA YOYOTE YA AINA YOYOTE ILE. EPSON NA WAGAVI WAKE HAWADHAMINI NA HAWATAWEZA KUDHAMINI UTENDAJI AU MATOKEO UNAYOWEZA KUPATA KWA KUTUMIA PROGRAMU HII. Epson haidhamini kwamba utendaji wa Programu hii hautakatizwa, hautakuwa na kasoro, hautakuwa na virusi au vijenzi vingine hatari au hatari za aina nyingine, au kwamba vipengele vya Programu hii vitatimiza mahitaji yako. Wajibu mmoja na wa kipekee wa Epson na suluhisho lako la kipekee la ukiukaji wa dhamana hii utakuwa aidha, kwa hiari ya Epson, kubadilisha media ya Programu au kurejesha pesa zako baada ya kurejesha Programu na Maunzi ya Epson. Ubadilishaji wowote wa Programu utakuwa chini ya dhamana kwa kipindi kinachosalia cha dhamana ya kwanza au kipindi cha siku thelathini (30), kipindi kile kirefu. Ikiwa sulusho lilitajwa hapa juu halitafaulu kwa sababu yoyote ile, wajibu wote wa Epson kwa ukiukaji wa dhamana una kikomo cha urejeshaji wa fedha zilizolipiwa Maunzi ya Epson. Epson haiwajibiki kwa cheleo la utendaji au kutofanya kazi kwa sababu isizoweza kudhibiti. Dhamani hii yenye Kikomo utakuwa batili ikiwa kasoro ya Programu kutasababishwa na ajali, matumizi mabaya, au matumizi kwa njia isiyofaa. DHAMANA NA SULUHISHO LENYE KIKOMO LILILOTAJWA HAPA JUU NI LA KIPEKEE NA LITATUMIWA BADALA YA YOTE MENGINE. EPSON INAKANUSHA DHAMANA ZOTE ZINGINE, AIDHA ZA WAZI AU DHANA, IKIJUMUISHA BILA KIKOMO, DHAMA ZOTE ZA KUTOKIUKA, UUZAJI, NA USAWA KWA MADHUMUNI FULANI. MAJIBU AU MAMLAKA MENGINE, HATA HIVYO, HAYARUHUSU KUTENGWA AU VIKOMO VYA DHAMANA ZA DHANA NA KATIKA MAJIBO HAYO, VIKOMO VILIVYOTAJWA HAPA JUU HUENDA VISITUMIKE KWAKO.

8.Kikomo cha Wajibu.
Kwa mujibu wa fungu 25 na/au 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), KWA KIWANGO CHA JUU KINACHORUHUSIWA NA SHERIA INAYOTUMIKA, EPSON AU WAGAVI WAKE HAWATAWAJIBIKA KWA HASARA ZOZOTE ZILE, ZIWE ZA MOJA KWA MOJA, ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA, MAALUM, ZINAZOHUSIANA NA TUKIO, AU HASARA ZA KIMATOKEO, ZIWEZI ZINATOKEA CHINI YA MKATABA, UTESI (IKIWA NI PAMOJA NA UTELEKEZAJI), WAJIBU MKALI, UKIUKAJI WA DHAMANA, UPOTOSHAJI, AU VINGINEVYO, IKIJUMUISHA BILA KIKOMO, HASARA AU KUPUNGUA KWA FAIDA YA BIASHARA, AU HASARA NYINGINE YA KIFEDHA, INAYOTOKANA NA MATUMIZI YA AU KUTOWEZA KUTUMIA PROGRAMU HII, AU YANAYOTOKANA NA MAKUBALIANO HAYA, HATA KAMA EPSON AU WAWAKILISHI WAKE WAMESHAURIWA KUHUSU UWEZEKANO WA HASARA KAMA HIZO. BAADHI YA MAJIMBO HAYARUHUSU KUONDOLEWA AU VIKOMO VYA HASARA KATIKA MIAMALA FULANI, NA KATIKA MAJIMBO HAYO, VIKOMO NA UTENGWAJI ULIO HAPA JUU HUENDA USITUMIKE.

9.Ununuaji wa Programu wa Serikali ya Marekani.
Fungu hili linatumika kwa ununuzi wote wa Programu hii wa au kwa Serikali ya Marekani (“Serikali”), au wa mkandarasi yoyote mkuu au mkandarasi mdogo (katika kiwango chochote) katika mkataba wowote, ruzuku yoyote, makubaliano yoyote ya ushirikiano, “muamala mwingine” (“OT”), au shughuli nyingine na Serikali. Kwa kupokea uwasilishaji wa Programu hii, Serikali, mkandarasi yoyote mkuu, na mkandarasi yoyote mdogo anakubali kwamba Programu hii inatimiza kuwa programu ya kimpyuta ya “kibiashara” ndani ya maana ya Sehemu 12 ya FAR, aya (b) ya Sehemu ndogo 27.405 ya FAR, au Sehemu ndogo 227.7202 ya DFARS, inavyotumika, na kwamba hakuna kanuni nyingine, au fungu la haki za data ya FAR au DFARS, itatumika kwa uwasilishaji wa Programu hii kwa Serikali. Alimradi, sheria na masharti ya Makubaliano haya yanasimamia matumizi na ufichuzi wa programu hii wa Serikali (na mkandarasi mkuu na mkandarasi mdogo), na inashinda sheria na masharti yoyote pinzani ya mkataba, ruzuku, makubaliano ya ushirikiano, OT, au shughuli zingine zinazohusiana na uwasilishaji wa Programu kwa Serikali. Ikiwa programu hii haitatimiza mahitaji ya Serikali, ikiwa Makubaliano haya hayalingani na sheria yoyote ya Shirikisho, au ikiwa sheria za FAR na DFARS zilizotajwa hapa juu hazitumiki, basi Serikali inakubali kurudisha Programu hii, ikiwa haijatumika, kwa Epson.

10.Uzuiaji wa Uhamishaji.
Unakubali kwamba Programu hii haitasafirishwa, kuhawilishwa au kuhamishwa nchi yoyote au kutumia kwa namna inayozuiwa na Sheria ya Usimamizi wa Uhamishaji ya Marekani au sheria, vikwazo, au kanuni zozote zingine za uhamishaji.

11.Makubaliano Kamili.
Kwa mujibu wa fungu 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), makubaliano haya ni makubaliano kamili katiya wahusika wanaohusiana na Programu hii na yanazidi maagizo yoyote ya ununuzi, mawasiliano, utangazaji, au uwakilishi wowote kuhusu Programu hii.

12.Makubaliano ya Kubana; Wanaokabidhiwa.
Makubaliano haya yatabana kwa, na kwa manufaa ya, wahusika wa makubaliano haya na warithi, wakabidhiwa na wawakilisho wako husika.

13.Ukomo; Marekebisho.
Ikiwa sheria yoyote katika makubaliano haya itagunduliwa kuwa batili au isiyoweza kutekelezwa na mahakamaya mamlaka halali (kama vile Fungu 22.8 na 22.9 ikiwa uko Markeani), haitaathiri uhalali wa usawa wa Makubaliano haya, yatakayoendela kuwa halali na kutekelezeka kulingana na sheria zake. Kwa mujibu wa fungu 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), makubaliano haya yanaweza kurekebishwa tu kwa maandiko yaliyotiwa sahihi na mwalikilishi aliyedhinishwa wa Epson.

14.Fidia.
Kwa mujibu wa fungu 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), unakubali kwamba utafidia na kutodai, na ukiagizwa na Epson, utaitetea Epson na wakurugenzi, maofisa, washikadau, wafanyakazi, na wakala wake kutokana na dhidi ya hasara, wajibu, uharibifu, gharama (ikijumuisha ada busara ya mawakili), vitendo, mashtaka, madai yanayotokana na (i) ukiukaji wowote wa wajibu wako katika Makubaliano haya au (ii) matumizi yoyote ya Programu hii au Maunzi ya Epson. Ikiwa Epson itakuambo uitetee katika mashtaka, au madai yoyote kama haya, Epson itakuwa na haki, kwa gharama yake, kushiriki katika ulinzi na wakili wake. Hutatatua madai yoyote ya wahusika wa tatu ambayo Epson inastahiki fidia bila idhini ya maandiko ya kabla ya Epson.

15.Usitishwaji.
Kwa mujibu wa fungu 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), bila ushirikina kwa haki zingine zozote ambazo Epson iko nazo, haki zako za leseni chini ya Fungu 1 lililo hapa juu na haki zako za dhamana chini ya Fungu 7 lililo hapa juu, zitasitishwa kiotomatiki baada ya kukosa kutii Makubaliano haya. Baada ya kusitishwa kwa haki hizi, unakubali kwamba Programu hii, na nakala zake zote, zitaharibiwa mara moja.

16.Uwezi na Mamlaka ya Kuingia katika Mkataba.
Kwa mujibu wa fungu 28 (ambalo linaweza kutumika kwako ukinunua bidhaa na huduma kutoka Epson nchini Australia), unakubali kwamba umefikisha umri wa kisheria wa kuwa mtu mzima katika jimbo au mamlaka unayoishi na una mamlaka yote husika ya kuingia katika Makubaliano haya, ikijumuisha, ikiwa inatumika, mamlaka ya mwajiri wako kuingia katika Makubaliano haya.

17.Faragha, Uchakataji wa Taarifa.
Programu hii inaweza kuwa na uwezo wa kuunganisha kwenye Wavuti ili kuhawilisha data kwenye na kutoka kwenye Kifaa chako. Kwa mfano, ukisakinisha Programu hii, Programu hii inaweza kusababisha Kifaa chako kutuma taarifa kuhusu Maunzi yako ya Epson, kama vile, muundo na nambari tambulishi, kitambulisho cha nchi, msimbo wa lugha, taarifa ya programu endeshi, na taarifa ya matumizi ya Maunzi ya Epson kwenye tovuti ya Wavuti ya Epson ambayo inaweza kurudisha taarifa ya ukuzaji au huduma kuonyeshwa kwenye Kifaa chako. Uchakataji wowote wa taarifa iliyotolewa kupitia Programu hii, utatekelezwa kulingana na sheria husika za ulizni wa data na Sera ya Epson iliyo katika https://global.epson.com/privacy/area_select_confirm_eula.html. Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika, kwa kukubali sheria za Makubaliano haya na kwa kusakinisha Programu hii, unakubali taarifa yako kuchakatwa na kuhifadhiwa katika na/au nje ya nchi yako ya makazi. Ikia kuna sera yoyote maalum ya faragha iliyo katika Programu hii na/au inayoonyeshwa wakati unatumia Programu hii (kwa mfano, kwa programu fulani tumizi), sera kama hivyo maalum ya faragha itatawala Sera ya Faragha ya Epson iliyotajwa hapa juu.

18.Tovuti za Wahusika wa Tatu.
Unaweza, kupitia matini hipa au viungo vingine vya kompyuta kutoka kwenye Programu hii, kufikia tovuti na kutumia huduma fulani ambazo hazidhibitiwi au kuendeshwa na Epson, lakini zinazodhibitiwa na wahusika wa tatu. Unakiri na kukubali kwamba Epson haiwajibiki kwa tovuti au huduma hizo za wahusika wa tatu, ikiwa ni pamoja na usahihi, ukamili, ufanisi wa muda, uhalali, utiifu wa hakimiliki, maadili, ubora, au vigezo vyovyote vingine. Tovuti/huduma hizi za wahusika wa tatu ziko chini ya sheria na masharti tofauti na unafikia na kutumia tovuti/huduma za wahusika wa tatu, utabanwa kisheria na sheria na masharti ya tovuti/huduma hizo. Sheria na masharti ya tovuti/huduma za wahusika wa tatu zitatawa kulingana na ufikiaji na matumizi yako ya tovuti/huduma hizo. Ingawa Epson inaweza kutoa kiungo cha tovuti/huduma ya wahusika wa tatu katika Programu, kiungo hicho sio idhini, mapendekezo, ufadhili au ushirikiano na Epson kwa tovuti/huduma hizo, maudhui yake, na wamiliki wake au watoa huduma wake. Epson inatoa viungo hivyo kwa marejeleo na manufaa yako. Alimradi, Epson haitoi uwakilishi wowote kwa tovuti/huduma hizo na haitoi usaidizi wowote kwa tovuti au huduma hizo za wahusika wa tatu. Epson haijajaribu taarifa, bidhaa au programu zozote zinazopatikana kwenye tovuti/huduma huzo na kwa hivyo haiwezi kutoa uwakilishi wowote. Unakubalia kwamba Epson haiwajibik kwa maudhui au utendaji wa tovuti/huduma hizo, na ni jukumu lako kuwa makini ili kuhakikisha kwamba chochote unachochagua hakina virusi, Trojani na vipengele vingine haribifu. Unawajibu wa kipekee wa kuamua kiwango ambacho unaweza kutumia maudhui yoyote kutoka kwenye tovuti/huduma zozote zingine ambazo unaelekezwa kutoka kwenye Programu hii.

(IKIWA UKO MAREKANI, MAFUNGU YANAYOFUATA 19-23 YANATUMIKA KWAKO)

19.Ununuaji wa Wino.
Kwa bidhaa fulani za printa ya Epson zinazouzwa Amerika Kaskazini, Programu hii inaweza pia kuonyesha chaguo la kununua wino kutoka Epson. Ukofya kwenye kitufe cha kununua, Programu hii itaelekeza Kifaa chako kuonyesha aina za katriji ya Maunzi ya Epson na viwango vya wino na kutoa taarifa nyingine kuhusu katriji zako, kama vile, rangi, ukubwa wa katriji zinazopatikana, na bei ya kubadilisha katriji za wino, unazoweza kununua mtandaoni.

20.Usasisho Unaoweza Kupakuliwa.
Pia unaweza kupakua usasisho au uboreshaji wa Programu kutoka tovuti ya Wavuti wa Epson ikiwa usasisho au uboreshaji huo unapatikana. Ikiwa unakubali kusakinisha Programu hii, uhawilishaji kwenye au kutoka kwenye Wavuti, na ukusanyaji na matumizi ya data, utafanywa kulingana na Sera ya Faragha ya wakati huo ya Epson, na kwa kusakinisha Programu unakubali kwamba Sera ya Faragha ya waati huo itasimamia shughuli hizo.

21.Akanti ya Epson na Ujumbe wa Ukuzaji.
Zaidi ya hayo, ukisakinishwa Programu hii na usajili Maunzi yako ya Epson na Epson, na/au uunde akaunti katika Duka la Epson, na bora uwe umetoka kubali chako kwa matumizi hayo, unakubali kwamba Epson inaweza kuchanganya data inayokusanywa kwa uhusiano wa usakinishaji wa Programu hii, usajili wa Maunzi yako ya Epson na/au uunfdaji wa akaunti yako ya Duka la Epson, ikiwa ni pamoja na taarifa ya kibinafsi na taarifa tambulishi isiyo ya kibinafsi, na matumizi ya data hiyo iliyochanganywa kutuma taarifa yako ya ukuzaji au huduma ya Epson. Ikiwa hutaki kutuma taarifa kuhusu Maunzi yako ya Epson au kupokea taarifa ya ukuzaji au huduma, utaweza kulemaza vipengele hivi kwenye mfumo wa Windows kupitia fungu la Inachunguza Mapendeleo katika kiendeshi. Kwenye programu endeshi ya Mac,unaweza kulamaza vipengele hivi kwa kusakinusha Epson Customer Research Participation katika Itafiti wa Epson na Low Ink Reminder.

22.MIZOZO, UPATANISHI UNAOBANA, NA UONDOAJI WA MASHTAKA NA UPATANISHI WA KIKUNDI

22.1Mizozo.
Sheria za Fungu hili 22 zitatumika kwa Mizozo yote kati yako na Epson. Neno “Mzozo” linatumiwa kuwa na maana kubwa zaidi inayoruhusiwa na sheria na inajumuisha mzozo, madai, mabishano au hatua kati yako na Epson inayotokana na au inayohusiana na Makubaliano haya Programu hii, Maunzi ya Programu, au muamala mwingine unaokuhusu wewe na Epson, uwe katika mkataba, dhamana, upotoshaji, ulaghai, utesi, utesi wa makusudi, masharti, kanuni, huumu, au katika misingi yoyote mingine ya kisheria au usawaziko. “MZOZO” HAUJUMUISHI MADAI YA UVUMBUZI, au kwa kihususa zaidi, madai au sababu ya kitendo cha (a) ukiukaji au kupunguza uzito wa nembo ya kibiashara, (b) ukiukaji wa hataza, (c) ukiukaji au matumizi mabaya ya hakimiliki, au (d) udanganyifu wa siri ya kibiashara (“Madai ya IP”). Wewe na Epson pia minakubali, bila kujali Fungu 22.6, kwamba mahakama, mpatanishi, anaweza kuamua kama madai au sababu ya mashtaka ya Madai ya IP.

22.2Upatanishi Unaobana.
Wewe na Epson munakubali kwamba Mizozo yote itatatuliwa kwa upatanishi unaobana kulingana na Makubaliano haya. UPATANISHI UNAMAANISHA KWAMBA UNAONDOA HAKI YAKO YA HAKIMU AU JOPO LA MAJAJI KATIKA MASHTAKA YA KOTINI NA HAKI ZAKO ZA RUFAA NI CHACHE. Kufuatilia Makubaliano haya, upatanishi unaobana utatekelezwa na JAMS, mamlaka ya upatanishi inayotambuliwa kitaifa, kulingana na kanuni yake ya utaratibu zinazotumika kwa mizozo inayohusiana na wateja, lakini bila kujumuisha sheria zozote zinazoruhusu muungano au mashtaka ya kikundi katika upatanishi (kwa maelezozaidi kuhusu utaratibu, angalia Fungu 22.6 lililo hapa chini). Wewe na Epson munaelewa na kukubali kwamba (a) Sheria ya Upatanishi ya Shirikisho (9 U.S.C. §1, et seq.) inasimamia utafsiri na utekelezaji wa Fungu hili 22, (b) Makubaliano haya yanakumbuka muamala katika biashara ya kati ya majibo, na (c) Fungu hili 22 litaendela hata baada ya kusitishwa kwa Makubaliano.

22.3Hatua na Notisi za Kabla ya Upatanishi.
Kabla ya kuwasilisha madai ya upatanishi, wewe na Epson munakubali kujaribu, kwa siku sitini (60), kutatua Mzozo wowote kwa namna isiyo rasmi. Ikiwa Epson na wewe hamtafikia makubaliano ya kutatua Mzozo ndani ya siku sitini (60), wewe au Epson inaweza kuanzisha hatua ya upatinishi. Lazima notisi kwa Epson itumwekwa: Epson America, Inc., KWA: Idara ya Sheria, 3131 Katella Ave. Los Alamitos, CA 90720 (“Anwani ya Epson”). Notisi ya Mzozo itatumwa kwako kupitia anwani ya mwisho kurekodiwa katika rekodi za Epson. Kwa sababu hii, ni muhimu kutuarifu ikiwa anwani yako itabadilika kuwa kututumia barua pepe kupitia EAILegal@ea.epson.com au kwa kutuandikia barua kwa Anwani ya Epson iliyo hapa juu. Nositi ya Mzozo itajumuisha jina la mtumaji, anwani yake na taarifa ya kuwasiliana naye, sababu za Mzozo hu, na suluhisho linaloagizwa (“Notisi ya Mzozo”). Baada ya kupokea Notisi ya Mzozo, Epson na wewe mutakubali kuchukua hatua kwa nia njema kutatua Mzozo huo kabla ya kuanza upatanishi.

22.4Mahakama ya Madai Madogo.
Bila kujali yaliyotajwa hapa juu, unaweza kuleta mashtaka ya kibinafsi katika mahakama ya madai madogo ya jimbo au manispaa yako ikiwa mashtaka hayo yako ndani ya mamlaka ya mahakama na yanasubiri tu katika mahaka hiyo.

22.5UONDOAJI WA MASHTAKA NA UPATANISHI WA KIKUNDI.
WEWE NA EPSON MUNAKUBALI KWAMBA KILA MHUSIKA ANAWEZA KUSHTAKI MZOZO DHIDI YA MHUSIKA HUYO MWINGINE TU KATIKA UWEZO WA MTU BINAFSI, NA SIO KAMA MSHTAKI AU MWANACHAMA WA KUKINDU KATIKA MASHTAKA YA KIKUNDI AU UWAKILISHAJI, IKIWA NI PAMOJA, LAKINI BILA KIKOMOKWA, MASHTAKA YA KIKUNDI YA SHIRIKISHO AU JIMBO, AU UPATINISHI WA KIKUNDI. KESI ZA MASHTAKA YA KUKUNDI, UPATANISHI WA KIKUNDI, MASHTAKA YA KIBINAFSI YA MWANASHERIA MKUU, NA MASHTAKA YOYOTE MENGINE AMBAYO MTU MWINGINE ANATENDA KAMA MWAKILISHI HAYARUHUSIWI. ALIMRADI, CHINI YA TARATIBU ZA UPATANISHI ZILIZOORODHESHWA KATIKA FUNGU HILI, MPATANISHI HATACHANGANYA AU KUUNGANISHA MASHTAKA YA ZAIDI YA MHUSIKA MMOJA BILA KIBALI CHA MAANDIKO KUTOKA KWA WAHUSIKA WOTE WAATHIRIKA WALIO KATIKA UPATANISHI HUO.

22.6Utaratibu wa Upatanishi.
Ikiwa wewe au Epson mutaanzisha upatanishi, upatanishi utasimamiwa na sheria za JAMS ambazo zinatumiwa wakati upatanishi unaripotiwa, isipokuwa sheria zozote zinazoruhusu upatanishi kwa misingi ya kikundi au uwakilishi (“Sheria za Jams”), zinazopatikana katika http://www.jamsadr.com au kwa kupiga simu kwa 1-800-352-5267, na katika sheria zilizowekwa katika Makubaliano haya. Mizozo yote itatatuliwa na mpatanishi mmoja asiyeegemea upande wowote, na wahusika wote wawili watakuwa na fursa busara ya kushiriki katika uteuzi wa mpatanishi. Mtananishi amebanwa na sheria za Makubaliano haya. Mpatanishi, na mahakama au wakala wowote wa ndani wa shirikisho au jimbo, ana mamkala ya kipekee kutatua mizozo yote inayotokana na au inayohusiana na utafsiri, utumiaji, utekelezaji au utungaji wa Makubaliano haya, ikiwa ni pamoja na madai yoyote ambayo Makubaliano haya yote au sehemu ya Makubaliano haya ni batili au sio halali. Bila kujali unaibishaji huu mpana wa mamlaka kwa mpatanishi, mahakama inaweza kuamua swali lenye kikomo la kama madai au sababu ya mashtaka ni ya Madai ya Uvumbuzi, ambayo hayajajumuishwa katika ufafanuzi wa “Mizozo” katika Fungu 22.1 hapa juu. Mpatanishi anapewa nguvu za kutoa usuluhisho wowote ule unapatikana katika mahakama chini ya sheria au usawa. Mpatanishi anaweza kukupatia fidia sawa na ile ya mahakama, na anaweza kutoa usuluhisho wa kutangazwa au amri ya kukomesha tu kwa mhusika anayeomba usuluhisho na kwa kiwango kinachohitajika kutoa usuluhisho unaostahiki kwa madai ya mhusika huyo. Wakati mwingine, gharama ya upatanishi inaweza kuzidi gharama ya mashtaka na haki ya ugunduzi inaweza kuwa na vikwazo zaidi katika upatanishi kuliko mahakamani. Uamuzi wa mpatanishi unabana na unaweza kuchukuliwa kama uamuzi katika mahakama yoyote ya mamlaka halali.

Unaweza kuchagua kujihusisha katika maulizo ya upatanishi kupitia simu. Maulizo ya upatanishi yasiyotekelezwa kupitia simu yatafanyika katika sehemu inayoweza kufikiwa kutoka makazi yako ya kwanza, au katika Kaunti ya Orange, California, kwa hiari yako.

a) Uanzilishaji wa Mashtaka ya Upatanishi.
Ikiwa wewe au Epson mutaamua kutatua Mzozo kwa njia ya upatanishi, nyote wawili munakubali utaratibu unaofuata:
(i) Kuandika Agizo la Upatanishi. Lazima agizo hili lijumuishe ufafanuzi wa Mzozo na kiasi cha fidia unachotaka kupokea. Unaweza kupata nakala ya Agizo la Upatanishi katika http://www.jamsadr.com (“Agizo la Upatanishi”).

(ii) Tuma nakala tatu za Agizo la Upatanishi, pamoja na ada inayofaa ya kuripoti, kwa: JAMS, 500 North State College Blvd., Suite 600 Orange, CA 92868, Marekani.

(iii) Tuma nakala moja ya Agizo la Upatanishi kwa mhusika huyo mwingine (anwani sawa na ile ya Notisi ya Mzozo), au vile wahusika walikubaliana.
b) Mpangilio wa Maulizo.
Wakati wa upatanishi, kiasi cha fidia yoyote inayotolewa haitafichuliwa kwa mpatanishi hadi baada ya mpatanishi aamue kiasi hicho, ikiwa kunacho, ambacho wewe au Epson inastahiki. Ugunduaji au ubadilishaji wa taarifa isiyo ya kibinafsi inayohusiana na Mzozo huo unaweza kuruhusiwa wakati wa upatanishi.
c) Ada ya Upatanishi.
Epson italipa, au (ikiwa unatumika) itakurejeshea, ada zote za kuripoti za JAMS na ada za mpatanishi kwa upatanishi wowote ulianzishwa (na wewe au Epson) kufuatilia sheria za Makubaliano haya.
d) Uamuzi Unaokupendelea.
Kwa Mizizo ambayo wewe au Epson munataka fidia ya $75,000 ua chache bila kujumuisha data na gharama za mawakili, ikiwa uamuzi wa mpatanishi unakupatia kiasi cha fidia zaidi ya ofa ya mwisho kuandikwa na Epson, ikiwa kunayo, kutatua Mzozo, Epson: (i) itakulipa $1,000 au kiasi cha uamuzi, kiasi cha juu; (ii) itakulipa mara mbili ya kiasi cha ada busara ya wakili wako, ikiwa kunayo; na (iii) itakurejeshea gharama zozote (ikiwa ni pamoja na ada na gharama za mashahidi wataalamu) ambayo wakili wako ataongeza kwa upelelezi, maandalizi, na kufuatilia Mzozo katika upatanishi. Isipokuwa unapokubaliana na Epson kwa maandiko, mpatanishi ataamua kiasi cha ada na gharama inayofaa kulipowa na Epson kulingana na Fungu hili 22.6d).
e) Ada za Wakili.
Epson haitadai ada na gharama za wakili kwa upatanishi wowote unaohusiana na Mzozo wa Makubaliano haya. Haki yako ya ada na gharama za wakili katika Fungu 22.6(d) hapa juu haipunguzi haki zako za ada na gharama za wakili katika sheria husika; bila kujali yaliyotajwa hapa juu, mpatanishi huenda asikupatie ada na gharama za wakili mara mbili.

22.7Kuchagua Kujiondoa.
Unaweza kuchagua kujiondoa kutoka kwa utaratibu wa upatanishi wa kibinafsi wa mwisho, unaobana, na uondoaji wa taratibu za mashtaka ya kikundi ya wawakilishi uliotajwa katika Makubaliano haya kwa kutumia barua kwenye Anwani ya Epson ndani ya siku thelathini (30) za wewe kutia sahihi kwenye Makubaliano haya (ikijumuisha bila kikomo kwa ununuzi, upakuzi, sakinishaji wa Programu au matumizi mengine husika ya Maunzi, bidhaa na huduma za Epson) inayotaja (i) jina lako, (ii) anwani yako ya barua, na (iii) ombi lako la kuondolewa kutoka kwa utaratibu wa upatanishi wa kibinafsi wa mwisho, unaobana, na uondoaji wa taratibu za mashtaka ya kikundi ya wawakilishi uliotajiwa katika Fungu hili 22. Ikiwa uamuzi wako wa kujiondoa utalingana na utaratibu uliotajwa hapa juu, sheria zingine zote zitaendelea kutumika, ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kutoa notisi kabla ya mashataka.

22.8Marekebisho ya Fungu 22.
Bila kujali sheria zozote zilizo katika Makubaliano haya kwa kinyume, wewe na Epson munakubali kwamba ikiwa Epson itafanya marekebisho yoyote ya siku zijazo kwa utaratibu wa utatuzi wa mzozo na sheria za uondoaji wa mashtaka ya kikundi (mbali na mabadiliko ya anwani ya Epson) katika Makubaliano haya, basi Epson itapata kibali chako kamili cha marekebisho husika. Ikiwa huyakubali marekebisho husika kabisa, unakubali kwamba upatanishi wa Mzozo wowote kati ya wahusika kulingna na lugha ya Fungu hili 22 (au kutatua mizozo kama inavyotolewa katika Fungu 22.7, ikiwa ulichagua kujiondoa bila kuchelewa ulipokubali Makubaliano haya kwa mara ya kwanza).

22.9Ukomo.
Ikiwa sheria yoyote ya Fungu hili 22 itaonekana kuwa haiwezi kutekelezwa, sheria hiyo itasitishwa na sehemu ya Makubaliano haya inayosalia ikiendelea kutumika kikamilifu. Yaliyotajwa hapa juu hayatumika kwa uzuiaji dhidi ya mashtaka ya kikundi au wawakilishi kama ilivyotajwa katika Fungu 22.5. Hii inamaanisha kwaamba ikiwa Fungu 22.5 litaonekana kuwa haliwezi kutekelezwa, Fungu lote 22 (lakini Fungu 22 pekee) litakuwa batili.

23.Kwa Wakazi wa New Jersey.
BILA KUJALI SHERIA ZOZOTE ZILIZOWEKWA KATIKA MAKUBALIANO HAYA, IKIWA SHERIA ZOZOTE ZILIZOWEKWA KATIKA FUNGU 7 AU 8 ZITAONEKANA KUWA HAZIWEZI KUTEKELEZWA, NI BATILI AU HAZIWEZI KUTUMIKA KATIKA SHERIA YA NEW JERSEY, BADI SHERIA YOYOTE KAMA HIYO HAITATUMIKA KWAKO LAKINI MAKUBALIANO MENGINE YOTE YATAENDELEA KUWABANA WEWE NA EPSON. BILA KUJALI SHERIA ZOZOTE KATIKA MAKUBALIANO HAYA, HAKUNA KITU KATIKA MAKUBALIANO HAYA KIMEKUSUDIWA, WALA KITACHUKULIWA AU KUDHANIWA, KUPUNGUZA HAKI ZOZOTE ZINAZOPATIKANA KWAKO CHINI YA MKATABA, DHAMANA NA SHERIA YA NOTISI YA MTEJA.

FUNGU ZIFUATAZO 24-36 ZA HATI HII ZINAWEZA KUTUMIKA KWAKO UKINUNUA BIDHAA AU HUDUMA AUSTRALIA (TAZAMA FUNGU 25 NA 28 ILI KUPATA TAARIFA ZAIDI KUHUSU WAKATI FUNGU HIZI ZINATUMIKA)

24.Ufafanuzi.
Kwa madhumuni ya Fungu zifuatazo 24-36 za Makubaliano haya, Sheria ya Watumiaji ya Australia inamaanisha Ratiba 2 ya Sheria ya Ushindani na Mtumiaji ya 2010 (Cth).

25.Kununua Bidhaa kama Mtumiaji.
Ukinunua Programu nchini Australia kama mtumiaji chini ya Sheria ya Watumiaji ya Australia, ambayo inaweza kujumuisha watu binafsi au biashara au mashirika mengine ya ukubwa wowote, Makubaliano haya yapo chini ya Fungu zifuatazo 26 na 27.

26.Sheria ya Watumiaji ya Australia.
Hakuna kitu chochote katika Makubaliano haya kinachotumika ambapo kitatenga, kuzuia au kurekebisha haki yoyote au suluhisho unaloweza kuwa nalo chini ya Sheria ya Watumiaji ya Australia ikiwa haki hiyo au suluhisho hilo haliwezi kutengwa, kuzuiwa au kurekebishwa kisheria.

Bila kujali kitu chochote kilicho kinyume katika Makubaliano haya, ukinunua bidhaa na huduma kutoka kwa Epson kama mtumiaji, zinazokuja na dhamana za kisheria chini ya Sheria ya Watumiaji ya Australia ambazo hazijatengwa na masharti mengine yoyote ya Makubaliano haya.
Dhamana za kisheria zinajumuisha (bila kikomo) yafuatayo:

Bidhaa lazima ziwe za ubora unaokubalika. Hii inamaanisha lazima:
-ziwe salama;
-zisiwe na kasoro;
-ziwe na muonekano au bidhaa iliyokamilika inayokubalika;
-zifanye kazi yote ambayo kwa kawaida mtu angetarajia zifanye;
-zifanane na mfano wowote wa onyesho au sampuli;
-kufaa kwa madhumuni ambayo Epson imekuwakilishia kuwa itayafikia;
-zifanane na maelezo ya bidhaa yaliyotolewa na Epson; na
-zikidhi dhamana yoyote ya wazi uliyotolewa na Epson wakati wa ununuzi kuhusu utendakazi, hali na ubora wao.
Huduma zinazotolewa na Epson lazima:
-zitolewe kwa uangalifu unaostahili na ujuzi au maarifa ya kiufundi;
-zifikie madhumuni au kutoa matokeo ambayo yamekubaliwa kutolewa; na
-ziwasilishwe ndani ya muda muafaka wa kutosha wakati hakuna tarehe ya mwisho iliyokubaliwa.
Kwa kiwango fulani Epson ikishindwa kutii dhamana ya watumiaji inayokuhusu chini ya Sheria ya Watumiaji ya Australia, una haki ya kutumia suluhisho kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Watumiaji ya Australia.

27.Ilani ya Dhamana na Suluhisho
Fungu la 7 halitatumika kwako. Fungu lifuatalo litatumika badala yake:

BIDHAA ZA EPSON HUJA NA DHAMANA AMBAZO HAZIWEZI KUTENGWA CHINI YA SHERIA YA MTUMIAJI YA AUSTRALIA. UNA HAKI YA KUBADILISHIWA AU KUREJESHEWA FEDHA KWA SABABU YA KASORO KUBWA NA FIDIA KWA HASARA AU UHARIBU MWINGINE WOWOTE UNAOTARAJIWA. PIA UNA HAKI YA KUREKEBISHIWA AU KUBADILISHIWA BIDHAA HIZO IKIWA BIDHAA SIO ZA UBORA UNAOKUBALIKA NA KASORO HIYO SIO KASORO KUBWA.

ISIPOKUWA KWAMBA HAKUNA KITU CHOCHOTE KATIKA FUNGU HILI KINACHOTENGA, KINACHOZUIA AU KUREKEBISHA DHAMANA, GARANTI AU SULUHISHO AMBAZO HAZIWEZI KUJUMUISHWA CHINI YA SHERIA YA MTUMIAJI YA AUSTRALIA: (1) PROGRAMU INATOLEWA “KAMA ILIVYO” NA BILA DHAMANA YOYOTE YA AINA YOYOTE; (2) EPSON NA WAGAVI WAKE HAWADHAMINI NA HAWAWEZI KUDHAMINI UTENDAKAZI AU MATOKEO UNAYOWEZA KUPATA KWA KUTUMIA PROGRAMU HII. (3) Epson haidhamini kwamba utendakazi wa Programu hii hautakatizwa, hautakuwa na kasoro, hautakuwa na virusi au vijenzi vingine hatari au hatari za aina nyingine, au kwamba vipengele vya Programu hii vitatimiza mahitaji yako (4) Epson haiwajibiki kwa cheleo la utendakazi au kutofanya kazi kwa sababu isizoweza kudhibiti. (5) EPSON INAONDOA DHAMANA ZOTE ZINGINE, AIDHA ZA WAZI AU ZA DHANA, IKIJUMUISHA BILA KIKOMO, DHAMANA ZOTE ZA KUKIUKA, UUZAJI, NA USAWA KWA MADHUMUNI FULANI.

28.Kununua Bidhaa chini ya Mkataba wa Mtumiaji au wa Biashara Ndogo.
Ikiwa:

(a) wewe ni mtu binafsi na unanunua Programu yote hasa kwa matumizi ya kibinafsi, ya nyumbani au kwa ajili ya matumizi; au
(b) makubaliano haya yanajumuisha mkataba wa biashara ndogo (kama neno hilo linavyofafanuliwa katika Sheria ya Watumiaji ya Australia mara kwa mara),

basi fungu zifuatazo 29 - 36 zitatumika kwako.

29.Kikomo cha Wajibu.
Fungu 8 halitatumika kwako. Fungu lifuatalo litatumika badala yake:

Kwa mujibu wa Fungu 25, HAKUNA TUKIO LOLOTE AMBALO SHIRIKA AU WAGAVI WAKE WATAWAJIBIKA KWA HASARA ZOZOTE ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA, MAALUM, ZINAZOHUSIANA NA TUKIO, AU HASARA ZA KIMATOKEO, IWE ZINAZOTOKEA CHINI YA MKATABA, UTESI (IKIWA NI PAMOJA NA UTELEKEZAJI) WAJIBU MKALI, UKIUKAJI WA DHAMANA, UWAKILISHAJI POTOFU, AU VINGINEVYO IKIWEMO BILA KIKOMO, HASARA AU KUPUNGUA KWA FAIDA YA BIASHARA, KUKATIZWA KWA BIASHARA, KUPOTEZA TAARIFA ZA BIASHARA, AU HASARA NYINGINE ZA KIFEDHA, ZINAZOTOKANA NA MATUMIZI YA PROGRAMU AU KUTOWEZA KUTUMIA PROGRAMU, AU KUTOKANA NA MAKUBALIANO HAYA, HATA KAMA SHIRIKA HILO AU MWAKILISHI WAKE WAMESHAURIWA KUHUSU UWEZEKANO WA HASARA KAMA HIZO.

30.Utoaji wa Leseni.
Wajibu wa kulipa Epson fidia kama ilivyobainishwa katika Fungu 1 (Utoaji wa Leseni) halitumiki kwako. Unakiri na kukubali kwamba unawajibika kwa kitendo chochote na kosa la watumiaji wengine unaowaruhusu kutumia Programu kana kwamba ni kitendo au kosa lako.

31.Uboreshaji na Usasisho.
Ikiwa Epson inasasisha Programu kiotomatiki chini ya Fungu 2 (Uboreshaji na Usasisho), unaweza kusitisha Makubaliano haya kwa maandiko bila dhima zaidi kwa Epson ikiwa kipengele muhimu cha Programu kitabadilishwa, kusimamishwa au kuondolewa (kama tokeo la urekebishaji wa hitilafu, viambatisho, uboreshaji, vipengele vya ziada au vipengele vilivyoboreshwa, programu-jalizi na matoleo mapya) kutoka kwa Programu na unaweza kuonyesha kuwa hii ina zaidi ya madhara madogo yanayokuathiri.

32.Makubaliano Kamili.
Fungu 11 (Makubaliano Kamili) halitatumika kwako.

33.Ukomo; Marekebisho.
Makubaliano haya yanaweza kurekebishwa tu ikiwa, pamoja na kurekebishwa kwa maandiko yaliyotiwa sahihi na, au mwakilishi aliyeidhinishwa wa, Epson, pia yanarekebishwa kwa maandiko yaliyotiwa sahihi na, au mwakilishi wako aliyeidhinishwa.

34.Fidia.
Fungu 14 (Fidia) halitatumika kwako.

35.Usitishwaji.
Fungu 15 (Usitishwaji) halitatumika kwako. Fungu lifuatalo litatumika badala yake:

Bila kuathiri haki zingine zozote za wahusika, kila mhusika anaweza kusitisha Makubaliano haya, kuanzia wakati anapompa mhusika mwingine notisi, ikiwa mhusika mwingine atashindwa kutii Makubaliano haya. Baada ya kusitisha, lazima uache kutumia Programu, na ni lazima nakala zake zote ziharibiwe mara hiyohiyo.

36.Uwezo na Mamlaka ya Kuingia katika Mkataba.
Pamoja na uwakilishi uliotoa katika Fungu 16 (Uwezo na Mamlaka ya Kuingia katika Mkataba), Epson inawakilisha kwamba ina mamlaka yote yanayohitajika ya kuingia katika Makubaliano haya.

2023