Ikiwa printa yako tayari inaonyeshwa katika "Printers & Scanners", chagua printa yako, na ubofye kitufe cha [–] ili uifute. Ongeza kiendeshaji cha printa na kiendeshaji cha faksi (kwa modeli zilizo na dhima ya faksi) kulingana na maelekezo yaliyo hapa chini.
Bofya kitufe cha[+].
Chagua Add Printer or Scanner.
Chagua printa yako ya Epson kutoka kwa orodha.
Chagua kiendeshaji kilichoipa printa yako jina.
Bofya Add.
Kagua jedwali lililo hapa chini, ili kuhakikisha kwamba umechagua inayo paswa.
Mbinu ya Muunganisho
|
Kiendeshaji cha Printa
|
Kiendeshaji cha Faksi
|
USB
|
EPSON XXXXXX
|
FAX XXXXXX (USB)
|
Mtandao
|
EPSONXXXXXX YYYYYY
|
FAX EPSONYYYYYY(IP) au FAX EPSONZZZ.ZZZ.ZZZ.ZZZ(IP)
|
* XXXXXX = jina la kifaa. YYYYYY = tarakimu 6 za anwani ya MAC. ZZZ.ZZZ.ZZZ.ZZZ = anwani ya IP
|
Kumbuka:
Ukishaongeza viendeshaji, huhitaji kuviongeza tena isipokua ukibadilisha mbinu ya muunganisho au utumie kifaa tofauti.
Hakikisha kifaa kimewashwa na kimeunganishwa ipasavyo kwenye kompyuta yako kupitia USB au muunganisho wa mtandao.
Inaweza kuchukua muda kutafuta kiendeshaji cha faksi. Subiri hadi kiendeshaji cha faksi kimeonyeshwa kwenye orodha, na uongeze kiendeshaji cha faksi kupitia taratibu hiyo moja.