Unganisha iPhone au iPad yako na printa moja kwa moja kupitia Wi-Fi Direct.



1  Chagua kwenye skrini ya mwanzo ya printa.

2  Teua Wi-Fi Direct.

3  Gusa Anza Kusanidi.

4  Gusa iOS.

Msimbo wa QR unaonyeshwa kwenye paneli dhibiti ya printa.

5  Endesha programu ya Kamera ya Kawaida ya iOS.

Huwezi kuunganisha ukitumia programu kuchanganua misimbo ya QR.

6  Changanua msimbo wa QR katika modi ya PICHA, na kisha uguse taarifa inayoonyeshwa ili uunganishe kwenye printa.

7  Badilisha kutoka programu ya kamera ya kawaida na uwashe programu ya uchapishaji ya Epson.

Ifuatayo »

  • Wakati hujui unachofaa kufanya baada ya kuchanganua msimbo wa QR ukitumia programu ya Kamera

Gusa ujumbe unaoonyeshwa wakati unachanganua msimbo wa QR.

Gusa [Jiunge].

Washa Epson iPrint, na kisha uchague printa.


  • Wakati ujumbe wa muunganisho haujaonyeshwa hata baada ya kuchanganua msimbo QR

Ikiwa ujumbe wa muunganisho haujaonyeshwa, unganisha kwa kuchagua [Vifaa Vingine vya OS].

Vifaa Vingine vya OS »

Toleo la iOS la iPhone au iPad yako huenda likawa la zamani, au huenda ukawa hujatumia programu ya kawaida ya Kamera. Pia, huwezi kuunganisha kwenye printa ukitumia programu ya kuchanganua misimbo ya QR.

Unaweza kuangalia toleo la iOS yako kwa kuchagua [Mipangilio] - [Jumla] - [Kuhusu]. Ili uweze kutumia kipengele hiki, toleo la iOS11 au lipya linahitajika.