Unataka Kuiweka Aje?

  • Kuunganisha kupitia kipanga njia cha pasi waya (inapendekezwa)

Hii ndiyo mbinu ya muunganisho ya mitandao ya nyumbani na kazini iliyounganishwa kupitia kipanga njia pasi waya. Tunapendekeza mbinu hii kwa sababu inakuwezesha kutumia huduma za Epson Connect zinazotumia Wavuti. Utahitaji nenosiri la kipanga njia chako pasi waya. Mbinu hii hukuwezesha kuweka mipangilio ya Wi-Fi ya printa kwa kutumia Epson iPrint.


  • Unganisha Moja kwa Moja (Wi-Fi Direct)

Hii ndiyo mbinu ya muunganisho wakati hutumii kipanga njia pasi waya nyumbani au kazini. Printa na kifaa mahiri zimeunganishwa moja kwa moja. Unaweza kuunganisha hadi vifaa nane mahiri. Kwa sababu Wi-Fi Direct ni mtandao wa ndani ambao hauunganishi kwenye Wavuti, huwezi kutumia huduma zinazotumia Wavuti. Unaweza kuunganisha tu wakati unatumia printa. Mbinu hii hukuwezesha kuweka mipangilio ya Wi-Fi Direct ya kifaa chako mahiri.


  • Unganisha kichapishi ambacho kimeunganishwa tayari kwenye mtandao wako

Wakati printa imeunganishwa kwenye mtandao, unganisha kifaa mahiri kwenye mtandao mmoja (SSID) na printa. Unaweza kutumia printa kutoka kwenye kifaa mahiri.

  • Wakati hujui jinsi ya kufanya mipangilio ya Wi-Fi kwa kifaa cha simu

Onyesha skrini ya mipangilio ya Wi-Fi kwa kifaa cha mkononi, chagua mtandao unaotaka kuunganisha, kisha ingiza nenosiri.

  • Wakati unatumia iPhone au iPad (kifaa cha iOS)

Chagua [Mipangilio] - [Wi-Fi] ili uonyeshe skrini ya Wi-Fi.
Washa Wi-Fi, na kisha uguse mtandao unaotaka kuunganisha kutoka kwenye orodha ya mtandao. Ingiza nenosiri kwenye skrini ya kuingiza nenosiri, na kishe uguse [Jiunge].

  • Wakati unatumia kifaa cha Android

Chagua [Mipangilio] - [Wi-Fi] ili uonyeshe skrini ya Wi-Fi.
Washa Wi-Fi, na kisha uguse mtandao unaotaka kuunganisha kutoka kwenye orodha ya mtandao. Ingiza nenosiri la mtandao, na kishe uguse [Unganisha].


  • Wakati hujui nenosiri la kipanga njia cha pasi waya

Angalia kama maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia cha pasi waya. Kwenye lebo, huenda nenosiri likawa limeandikwa “Encryption Key”, “XXX Key”, na kuendelea. Ikiwa unatumia kipanga njia cha pasi waya katika mipangilio yake chaguo-msingi, nenosiri lililoandikwa kwenye lebo ndiyo linalotumika. Ikiwa huwezi kupata maelezo yoyote, angalia hati zilizotolewa na kipanga njia cha pasi waya.


  • Wakati kifaa cha rununu kimeunganishwa kwenye kipanga njia maalum cha rununu

Wakati una kipanga njia cha pasi waya (eneo la kufikia) cha kompyuta yako, unganisha kifaa mahiri na printa kwake. Wakati huna kipanga njia cha pasi waya, unganisha printa kwenye kipanga njia cha kifaa cha mkononi ambacho kifaa mahiri kimeunganishwa kwake.
Wakati printa haijaunganishwa kwenye mtandao, chagua “Kuunganisha kupitia kipanga njia cha pasi waya”. Wakati kimeunganishwa kwenye mtandao, chagua “Unganisha kwenye Printa ambayo imeunganishwa kwenye Mtandao”.


  • Wakati hutaki kuunganisha kifaa mahiri kwenye mtandao wa Wi-Fi (SSID) ambao printa imeunganishwa

Unganisha printa na kifaa mahiri moja kwa moja ukitumia Wi-Fi Direct. Unaweza kutumia printa kupitia muunganisho wa Wi-Fi ukitumia kipanga njia cha pasi waya na kwa muunganisho wa moja kwa moja kupitia Wi-Fi Direct.


  • Ikiwa unatumia kuunganisha (kushiriki mtandao) kwenye kifaa cha mkononi

Huwezi kuunganisha kwenye printa kutoka kwenye kifaa maizi wakait unatumia ufungaji kwenye kifaa maizi. Lemaza ufungaji, na kisha uunganishe kwenye printa.
Wakati printa haijaunganishwa kwenye mtandao, chagua “Kuunganisha kupitia kipanga njia cha pasi waya”. Wakati kimeunganishwa kwenye mtandao, chagua “Unganisha kwenye Printa ambayo imeunganishwa kwenye Mtandao”.