-
Wakati hujui jinsi ya kufanya mipangilio ya Wi-Fi kwa kifaa cha simu
Onyesha skrini ya mipangilio ya Wi-Fi kwa kifaa cha mkononi, chagua mtandao unaotaka kuunganisha, kisha ingiza nenosiri.
-
Wakati unatumia iPhone au iPad (kifaa cha iOS)
Chagua [Mipangilio] - [Wi-Fi] ili uonyeshe skrini ya Wi-Fi.
Washa Wi-Fi, na kisha uguse mtandao unaotaka kuunganisha kutoka kwenye orodha ya mtandao. Ingiza nenosiri kwenye skrini ya kuingiza nenosiri, na kishe uguse [Jiunge].
-
Wakati unatumia kifaa cha Android
Chagua [Mipangilio] - [Wi-Fi] ili uonyeshe skrini ya Wi-Fi.
Washa Wi-Fi, na kisha uguse mtandao unaotaka kuunganisha kutoka kwenye orodha ya mtandao. Ingiza nenosiri la mtandao, na kishe uguse [Unganisha].
-
Wakati hujui nenosiri la kipanga njia cha pasi waya
Angalia kama maelezo yameandikwa kwenye lebo ya kipanga njia cha pasi waya. Kwenye lebo, huenda nenosiri likawa limeandikwa “Encryption Key”, “XXX Key”, na kuendelea. Ikiwa unatumia kipanga njia cha pasi waya katika mipangilio yake chaguo-msingi, nenosiri lililoandikwa kwenye lebo ndiyo linalotumika. Ikiwa huwezi kupata maelezo yoyote, angalia hati zilizotolewa na kipanga njia cha pasi waya.
-
Wakati kifaa cha rununu kimeunganishwa kwenye kipanga njia maalum cha rununu
Wakati una kipanga njia cha pasi waya (eneo la kufikia) cha kompyuta yako, unganisha kifaa mahiri na printa kwake. Wakati huna kipanga njia cha pasi waya, unganisha printa kwenye kipanga njia cha kifaa cha mkononi ambacho kifaa mahiri kimeunganishwa kwake.
Wakati printa haijaunganishwa kwenye mtandao, chagua “Kuunganisha kupitia kipanga njia cha pasi waya”. Wakati kimeunganishwa kwenye mtandao, chagua “Unganisha kwenye Printa ambayo imeunganishwa kwenye Mtandao”.
-
Wakati hutaki kuunganisha kifaa mahiri kwenye mtandao wa Wi-Fi (SSID) ambao printa imeunganishwa
Unganisha printa na kifaa mahiri moja kwa moja ukitumia Wi-Fi Direct. Unaweza kutumia printa kupitia muunganisho wa Wi-Fi ukitumia kipanga njia cha pasi waya na kwa muunganisho wa moja kwa moja kupitia Wi-Fi Direct.
-
Ikiwa unatumia kuunganisha (kushiriki mtandao) kwenye kifaa cha mkononi
Huwezi kuunganisha kwenye printa kutoka kwenye kifaa maizi wakait unatumia ufungaji kwenye kifaa maizi. Lemaza ufungaji, na kisha uunganishe kwenye printa.
Wakati printa haijaunganishwa kwenye mtandao, chagua “Kuunganisha kupitia kipanga njia cha pasi waya”. Wakati kimeunganishwa kwenye mtandao, chagua “Unganisha kwenye Printa ambayo imeunganishwa kwenye Mtandao”.