Unataka Kuiweka Aje?

  • Unganisha Moja kwa Moja (Wi-Fi Direct)

Hii ndiyo mbinu ya muunganisho wakati hutumii kipanga njia pasi waya nyumbani au kazini. Printa na kifaa mahiri zimeunganishwa moja kwa moja. Unaweza kuunganisha hadi vifaa nane mahiri. Kwa sababu Wi-Fi Direct ni mtandao wa ndani ambao hauunganishi kwenye Wavuti, huwezi kutumia huduma zinazotumia Wavuti. Unaweza kuunganisha tu wakati unatumia printa. Mbinu hii hukuwezesha kuweka mipangilio ya Wi-Fi Direct ya kifaa chako mahiri.

  • Wakati hujui jinsi ya kufanya mipangilio ya Wi-Fi kwa kifaa cha simu

Onyesha skrini ya mipangilio ya Wi-Fi kwa kifaa cha mkononi, chagua mtandao unaotaka kuunganisha, kisha ingiza nenosiri.

  • Wakati unatumia iPhone au iPad (kifaa cha iOS)

Chagua [Mipangilio] - [Wi-Fi] ili uonyeshe skrini ya Wi-Fi.
Washa Wi-Fi, na kisha uguse mtandao unaotaka kuunganisha kutoka kwenye orodha ya mtandao. Ingiza nenosiri kwenye skrini ya kuingiza nenosiri, na kishe uguse [Jiunge].

  • Wakati unatumia kifaa cha Android

Chagua [Mipangilio] - [Wi-Fi] ili uonyeshe skrini ya Wi-Fi.
Washa Wi-Fi, na kisha uguse mtandao unaotaka kuunganisha kutoka kwenye orodha ya mtandao. Ingiza nenosiri la mtandao, na kishe uguse [Unganisha].